Serikali ya Tanzania yatakiwa kujenga maabara za TEHAMA katika kila shule
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Oran Njeza ameiagiza Ofisi ya Rais- TAMISEMI kuhakikisha inajenga maabara za TEHAMA katika kila shule ili wanafunzi wapate ujuzi kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia duniani. Ameyasema hayo Mei 21, 2024 kwenye kikao cha kujengewa uwezo wajumbe wa kamati hiyo kuhusu ufundishaji mubashara uliofanyika…
