Home VIWANDAUZALISHAJI Mabadiliko sekta ya utalii kuinua uchumi

Mabadiliko sekta ya utalii kuinua uchumi

0 comments 319 views

Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerewa amesema kuwa atahakikisha wanafanya mabadiliko na mapinduzi makubwa katika sekta ya utalii ili ichangie zaidi uchumi wa nchi.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Pindi Chana.

‘’Tunahifadhi na kutangaza utalii nchini. Lakini pia twende tukadhibiti ujangili tunataka tudhibiti kwelikweli ili kuhakikisha kwamba vitendo vya hovyo hovyo havitokei. Na mimi kwenye kipindi changu sitataka kusikia vitendo vya hovyo hovyo,’’ amesema Mchengerwa.

Aidha, Mchengerwa ameagiza kupatiwa taarifa za idara na taasisi za Wizara ifikapo Jumatatu, Februari, 20, 2023 ili aweze kuzipitia.
‘’Nataka kupitia taarifa hizi halafu tutaitana kwa ajili ya kupanga kazi tuweze kujua ndani ya kipindi cha miezi miwili tumekwendaje kwenye Wizara yetu ili tuweze kutimiza zile ndoto ambazo tunazo za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,’’ ameongeza Mchengerwa.
Waziri huyo pia amehimiza ushirikiano baina yake na Waziri aliyekuwepo Balozi Dkt. Pindi Chana.


Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa dhamana ya kusimamia Wizara ya Maliasili na Utalii akieleza kuwa pamoja na kwamba sasa yupo Wizara ya Utamduni Sanaa na Michezo ataendeleza ushirikiano ili kuhakikisha Wizara zote mbili zinafanya kazi kwa pamoja.

Pesatu ni jukwaa la habari, elimu ya kifedha, na ujasiriamali Tanzania. Tunakuletea taarifa mpya za biashara, uwekezaji, ajira, kilimo, mitindo, na burudani, pamoja na mwongozo wa kufanikisha mafanikio yako. Kwa makala zetu, mwongozo wa vitendo, na taarifa za hivi punde, tunasaidia wajasiriamali, vijana, na jamii kupata maarifa yanayoweza kubadilisha maisha yao na kuongeza fursa za kifedha.

Jarida la Habari

PESATU – Haki Zote Zimehifadhiwa. Imetengenezwa na Mediapix Limited