Rais Samia aridhia Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa kilimo
Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilimo utakaohusisha viongozi, watu mashuhuri na wadau takribani 3,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia mkutano huo kufanyika nchini Tanzania mwaka 2023. Taarifa hiyo inabainisha kwamba aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam…
