Utalii kuchangia Dola bilioni sita ifikapo 2025
Serikali ya Tanzania imesema imedhamiria kufikisha watalii milioni tano na sekta hiyo kuchangia mapato si chini ya dola bilioni sita ifikapo mwaka 2025. Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Saba ya Swahili International Tourism Expo – S!TE, 2023 yaliyofanyika Mlimani City, jijini Dar es Salaam. “Mmemsikia…
