WhatsApp Image 2023 10 25 at 13.52.39

Vikwazo nane vyaondolewa Tanzania, Zambia, vyabaki 16

Tanzania na Zambia zimekubaliana kuendelea kuondoa vikwazo mbalimbali vya kikodi na visivyo vya kikodi ambapo mpaka sasa vikwazo nane vimeondolewa kati ya 24 vilivyoainishwa na serikali hizo mbili. Makubaliano hayo ni pamoja na kuondoa urasimu, kuweka mazingira rahisi ya ufanyaji biashara, kuitumia vyema miundombinu inayounganisha nchi hizo na kuruhusu muingiliano wa watu. Hayo yamejadiliwa mjini…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 10 18 at 12.07.51

Tanzania kukuza sekta ya utalii

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeonyesha utayari wa kuendelea kuimarisha masuala ya uwekezaji, mafunzo na matumizi ya teknolojia katika kukuza sekta ya utalii kwa kufanyia kazi miongozo inayotolewa na Shirika la Utalii Duniani (UNWTO). Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Jasmine Kairuki amesema hayo baada ya kushiriki Jukwaa la Uwekezaji (Global Investment Forum)…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 10 11 at 16.01.32 1

Rais Samia akaribisha wawekezaji wa India

Rais Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji wa India kuja kuwekeza Tanzania akiahidi mazingira rafiki ya biashara na maendeleo ya uchumi. Mkuu huyo wa nchi, ameyasema hayo New Delhi wakati akizungumza na wawekezaji katika jukwaa la biashara na uwekezaji la Tanzania-India katika ziara yake ya siku tatu nchini India. Rais Samia amesema Tanzania inatekeleza maendeleo na…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 08 31 at 13.52.28

Kampuni ya Urusi kununua matunda Tanzania

Kampuni ya Magnit ya nchini Urusi imeeleza nia ya kununua bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania ikiwemo matunda. Hayo yameelezwa katika mkutano ulioratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kati ya kampuni hiyo na kampuni za Tanzania. Mwakilishi wa Kampuni hiyo ameeleza kuwa wanayo nia ya kununua bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania ikiwemo ndizi, nanasi, embe,…

Soma Zaidi
Enable Notifications OK No thanks