Home BIASHARA Fahamu jinsi ya kukuza biashara ndogo

Fahamu jinsi ya kukuza biashara ndogo

0 comments 341 views

Kukuza biashara ndogo inahitaji mpango mkakati mzuri, kuitangaza, usimamizi wa fedha, na kuzingatia wateja wako.

Weka malengo na mpango yako

Weka malengo mahususi (yaliyo wazi, yanayoweza kupimika na yanayowezekana. Hapa usiweke malengo ya vitu ambavyo havitaweza kutokea.

Jua kile unachofanya na kiwe kinakutofautisha na wafanyabiashara wengine, weka sababu kwa nini wateja wanunue kwako na sio kwa wafanya biashara wengine.

Pia fanya uchunguzi juu ya ushindani/wapinzani wako pamoja na mwennendo mzima wa soko.

Boresha bidhaa/huduma zako

Hapa unapaswa kupata maoni kutoka kwa wateja wako ili uweze kuboresha na kuwapatia kile wanachokitaka Zaidi.

Hakikisha ubora wa bidhaa/huduma yako ili uweze kujenga uaminifu. Pia unaweza kuongeza huduma mbalimbali ili mteja akija kwako apate angalau vitu vingi kwa wakati mmoja.

Kukuza biashara ndogo inahitaji mpango mkakati mzuri pesatu.co.tz

Baadhi ya vifaa vya ujenzi. Picha|Mtandao

Wajue wateja wako

Boresha bidhaa na huduma zako. Hii itasaidia kuwavutia wateja wako na kupata mafanikio. Kufanya utafiti kujua ni nini hasa mteja anahitaji ni njia rahisi ya kupata wateja.

Boresha huduma kwa wateja

Huduma bora kwa wateja ni nguzo muhimu katika biashara. Kukosekana kwa huduma bora kunaweza kusababisha kutowaridhisha wateja wako hata kama una bidhaa nzuri. Kwenye biashara hii huwafanya wateja wajisikie wakipekee.

Jenga uaminifu

Itachukua muda kuwashawishi wateja kununua bidhaa zako. Lakini kuwafanya wanunue pekee haitoshi. Unatakiwa kuwa mwaminifu ukijua kuwa kuna wapinzani katika biashara ambao wanaweza kutoa bidhaa bora Zaidi. Inakubidi kuwa makini Zaidi wasije wakavutiwa na kuchukuliwa kirahisi na wapinzani wako katika biashara.

Matumizi ya mitandao ya kijamii

Mitandao ya kijamii ni nguzo muhimu katika ufanyaji wa biashara. Mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter na mingine inawafikia mamia na maelfu ya watu kwa wakati mmoja. Hakikisha unaitumia kutangaza na kuonesha bidhaa zako. Kupitia mitandao ya kijamii, utaweza kusikiliza maoni ya wateja kutakufanya ujue ni nini wateja wanataka na ni nini cha kuboresha katika biashara yako.

Tengeneza Tovuti yako: Hakikisha inaonekana kwenye Google, ina kasi, na inafaa kwa simu.

Kwenye mitandao hiyo unaweza kuweka taarifa kama picha, video ama maelekezo yanayohusiana na bidhaa au huduma unayotoa.

Katika mitandao ya kijamii pia unaweza kutangaza ofa mbalimbali na wateja wakaweza kuziona kwa urahisi bila kufika dukani. Hapa biashara ikikua unaweza pia kutumia matangazo ya kulipia kama ya Facebook au kushirikiana na watu maarufu wenye wafuasi wengi kukutangazia biashara yako.

Hii pia itakusaidia kuwajua vema wateja na kutimiza matakwa yao.

Kukuza biashara ndogo inahitaji mpango mkakati mzuri pesatu.co.tz

Boresha uzoefu wa mteja

Toa huduma bora (jibu maswali haraka pale wanapouliza, wekeza kwao. Pia omba maoni kutoka kwao.

Panua njia za mauzo

Hapa unaweza kuuza kwenye mitandao ya biashara (kama vile Jumia n.k.) au katika maduka makubwa kama vile super makerts.

Soma: Njia Kuu 5 za kukuza biashara

Simamia fedha kwa uangalifu

Fuatilia mapato na matumizi na upunguze matumizi yasiyo ya lazima.

Rudisha faida kwenye bidhaa inayopendwa na kununuliwa Zaidi. Kwa mfano unauza nguo za kike na kiume, hapo nguo za kike zikawa ndio zinazonunuliwa zaidi, basi katika faida yako wekeza Zaidi kwenye nguo za kike.

Kama utahitaji kuikuza Zaidi unaweza kutafuta mkopo au wawekezaji wa kushirikiana nao.

Hudhuria warsha mbalimbali na kujenga mtandao wa biashara

Ukipata nafasi ya kuhudhuria warsha au mikutano mbalimbali inayohusu maswala ya biashara usiipoteze.

Hii ni fursa ya kukuza mtandao wako wa biashara na kujenga mahusiano mapya. Unapokutana na wafanyabiashara wengine itakusaidia kujifunza mambo tofauti na kupata ujuzi wa kukuza na kuboresha biashara yako kwa viwango vya juu.

Wajasiriamali wengi huwa hawaitumii nafasi hii. Unaweza ukakutana na wateja wapya, wafanyakazi n ahata wawekezaji.

Kua polepole lakini imara

Jaribu masoko mapya (eneo jipya au aina mpya ya wateja) huku ukiendelea na eneo lwa mwanzo.

Ajiri wafanyikazi wazuri kadri biashara inavyokua huku ukiendelea kujifunza na kufanya maboresho kila mara.

Chunguza takwimu muhimu (mauzo, gharama ya kupata mteja, na wateja wanaorudi). Pia unaweza kubadili mbinu kulingana na soko.

Kua mwenye kujifunza kila siku (soma, na ujifunze kwa wengine itakusaidia kuongeza maarifa na kukuza biashara yako kwa viwango vya juu.

Soma: Zingatia haya kukuza biashara yako

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!