TRA YAZIDI KUKAZA MWENDO DHIDI YA UKWEPAJI WA KODI NCHINI

TRA yazidi kukaza mwendo dhidi ya ukwepaji wa kodi nchini, Katika juhudi za kuimarisha uchumi wa taifa na kuongeza mapato ya Serikali, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea kuchukua hatua madhubuti dhidi ya watu binafsi na makampuni yanayojihusisha na vitendo vya ukwepaji wa kodi.

Hatua hizi ni sehemu ya mkakati mpana wa kuhakikisha kila mdau anatimiza wajibu wake wa kikatiba wa kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.

Kwa mujibu wa TRA, ukwepaji wa kodi ni mojawapo ya changamoto kubwa zinazoathiri ukusanyaji wa mapato, hali inayosababisha Serikali kukosa rasilimali muhimu kwa ajili ya kugharamia huduma za jamii kama afya, elimu, maji na miundombinu.

TRA YAZIDI KUKAZA MWENDO DHIDI YA UKWEPAJI WA KODI NCHINI - pesatu.co.tz

Moja ya hatua muhimu zinazochukuliwa na TRA ni kuimarisha matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika usajili wa walipakodi, utoaji wa risiti za kielektroniki (EFD), pamoja na uwasilishaji wa taarifa za kodi kwa njia ya mtandao.

Mifumo hii imeongeza uwazi na kupunguza mianya iliyokuwa ikitumika na wakwepa kodi kuficha mapato halisi.

Aidha, TRA imeongeza ukaguzi wa mara kwa mara katika maeneo ya biashara, viwandani na katika mipaka ya nchi ili kudhibiti magendo na biashara zisizo halali. Ukaguzi huu umeambatana na hatua kali za kisheria dhidi ya wanaobainika kukwepa kodi, ikiwemo kutozwa faini, kulipa kodi iliyokwepwa pamoja na riba, na katika baadhi ya matukio kufikishwa mahakamani.

Sambamba na hatua za kisheria, TRA imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari. Kupitia semina, kampeni za vyombo vya habari na mikutano na wafanyabiashara, mamlaka hiyo imekuwa ikisisitiza kuwa kodi si adhabu bali ni mchango wa moja kwa moja katika maendeleo ya taifa.

TRA YAZIDI KUKAZA MWENDO DHIDI YA UKWEPAJI WA KODI NCHINI - pesatu.co.tz

TRA pia imeimarisha ushirikiano na taasisi nyingine za Serikali, zikiwemo vyombo vya dola na mamlaka za serikali za mitaa, ili kubadilishana taarifa na kubaini kwa haraka vitendo vya ukwepaji wa kodi.

TRA YAZIDI KUKAZA MWENDO DHIDI YA UKWEPAJI WA KODI NCHINI: Ushirikiano huu umeongeza ufanisi katika kubaini wakwepa kodi wakubwa na mitandao ya ukwepaji wa mapato.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya utendaji kazi wa TRA kwa kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2025/2026 mkoani Arusha,Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda anasema TRA itaendelea kupambana na watu wanaojihusisha na vitendo vya ukwepaji wa kodi kwa kudhibiti mianya inayotumika kukwepa kodi.

Anasema TRA haitavumilia vitendo vyovyote vya ukwepaji wa kodi kufanyika nchini.

TRA YAZIDI KUKAZA MWENDO DHIDI YA UKWEPAJI WA KODI NCHINI - pesatu.co.tz

Anasema miongoni mwa hatua watakazochukua ni kuimarisha mipaka, kuzuia magendo na kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa jamii sambamba na elimu ya magendo.

Sambamba na kupambana na wakwepaji kodi Kamishna Mkuu anasema wamejipanga kuongeza wigo wa kodi kwa kusajili walipakodi wapya wakiwemo wafanyabiashara ambao bado hawajaingia katika mifumo ya kulipa kodi.

Anasema TRA itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu kama ilivyo jadi yake kwa kuwasikiliza walipakodi, kuwezesha biashara zao na kutatua changamoto zinazowakabili.

TRA YAZIDI KUKAZA MWENDO DHIDI YA UKWEPAJI WA KODI NCHINI - pesatu.co.tz

Aidha Mwenda anawataka watumishi wa TRA kuendelea kufanya kazi kwa weledi na bidii ili kuweza kuleta matokeo chanya katika ukusanyaji wa Mapato ya Serikali kwa Nusu ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2025/26.

Kamishna Mkuu Mwenda anasema kazi ya kukusanya kodi ni ya watumishi wote na siyo maafisa kodi pekee hivyo kila mtumishi wa TRA anapaswa kuhakikisha anatumia ubunifu, weledi na kuzingatia maadili ili kutimiza malengo ya TRA ya kukusanya Shilingi Trilioni 36.066 katika Mwaka wa Fedha 2025/26.

Anafafanua kua ni matumaini yake kuiona TRA inakusanya kodi kwa ufanisi na hatimaye kulifanya Taifa kujitegemea kupitia kodi zake.

“Na mimi ninatamani siku moja TRA iiwezeshe nchi yetu kuweza kujitegemea.”anasema Kamishna Mkuu Mwenda.

Akizungumza kuhusu mikakati ya ukusanyaji kwa Nusu ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2025/26 Kamishna Mkuu Mwenda anasema TRA imejidhatiti kuhakikisha inaendelea kutumia mifumo katika ukusanyaji wa kodi huku akiutaja mfumo wa IDRAS ambao utaanza rasmi Febuari 9, 2026.

Enable Notifications OK No thanks