Vijana na biashara ya kuku choma Dar
Ukipita maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam hasa nyakati za usiku, utawaona vijana wakifanya biashara ya kuuza kuku choma kandokando mwa barabara. Biashara hii imeshamiri na imewasaidia vijana wengi kujiajiri na kujipatia kipato. Watu wengi wanapotoka makazini na kwenye pilika pilika za kila siku, hupitia kitoweo hicho cha kuku choma kwa ajili ya mlo. Wengine…
