BoT kuja na mwongozo kutatua malalamiko ya watumiaji huduma za fedha
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iko mbioni kuandaa mwongozo utakaoainisha utaratibu wa kufuatwa katika kutatua malalamiko ya watumiaji wa huduma za fedha. Kaimu Mkurugenzi wa Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha Sadiki Nyanzowa, amesema mwongozo huo unalenga kuongeza ufanisi wa kushughulikia malalamiko hayo pamoja na kuleta usawa wa namna ya kushughulikia malalamiko kwa watoa huduma…
