Screen Shot 2025 04 30 at 2.15.38 PM

Gavana Tutuba akutana na Balozi wa Uingereza

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),  Emmanuel Tutuba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Marianne Young, katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam, tarehe 29 Aprili 2025. Katika mazungumzo hayo, Gavana Tutuba alieleza kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika licha ya changamoto mbalimbali za kiuchumi duniani. Alibainisha kuwa…

Soma Zaidi
Screen Shot 2025 04 29 at 3.14.08 PM

Afrika yaaswa kuimarisha ukusanyaji rasilimali za ndani kukabili misaada inayopungua

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Sauda Msemo, amezitaka serikali za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara kuimarisha ukusanyaji wa rasilimali za ndani ili kupunguza utegemezi mkubwa kwa misaada ya kigeni inayopungua. Akizungumza Aprili 28, 2025 katika mjadala ulioandaliwa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2025 04 28 at 15.34.21

Waziri Mkuu aagiza ufuatiliaji wa watendaji Vyama vya Ushirika

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo iimarishe na kufanya ufuatiliaji wa watendaji wa Vyama vya Ushirika ili wazingatie maadili ya utumishi wa ushirika, uwazi, uwajibikaji na utawala bora, na hivyo kuwavutia wanachama na wawekezaji. Pia Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo, pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika, iharakishe na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa…

Soma Zaidi
Screen Shot 2025 04 25 at 11.18.47 AM

Afrika yashauriwa kuweka mikakati kukabiliana na mabadiliko ya sera za kiuchumi

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amezishauri nchi za Afrika kuweka mikakati ya kufanya uwekezaji na biashara ndani ya Bara la Afrika ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya sera za kiuchumi zinazojitokeza hivi sasa duniani. Dkt. Nchemba ametoa ushauri huo jijini Washington D.C, nchini Marekani wakati akichangia taarifa ya Mwaka ya utekelezaji ya majukumu…

Soma Zaidi
Screen Shot 2025 04 25 at 1.59.37 PM

Kutofahamu thamani ya uwekezaji changamoto kampuni kutoorodheshwa Soko la Hisa DSM

Serikali imesema kuwa Kampuni ambazo hazijaorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) hukutana na changamoto za kutofahamu thamani halisi ya uwekezaji kutokana na kukosekana kwa ukwasi wa hisa zao. Hayo yalisemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande  wakati akijibu swali la Mbunge wa Geita Mjini, Constantine John…

Soma Zaidi
Screen Shot 2025 04 24 at 3.56.51 PM

Tanzania yapiga marufuku mazao ya Afrika Kusini, Malawi

Tanzania imepiga marufuku uingizwaji wa mazao yoyote ya kilimo kutoka Afrika ya Kusini na Malawi kuingia nchini Tanzania. Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametoa tamko hilo la serikali ya Tanzania Aprili 23, 2024. “Kama waziri wa Kilimo sijapokea notisi yoyote, mazungumzo yanaendelea na yanaongozwa na Waziri wetu wa Mambo ya Nje, lakini wakati mazungumzo yanaendelea…

Soma Zaidi
Enable Notifications OK No thanks