Tutaendelea kuunga mkono wawekezaji kwenye kilimo: Bashe
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Serikali itaendelea kuunga mkono wawekezaji wanaoonesha nia ya kuwekeza kwenye uongezaji thamani wa zao la alizeti hususan katika kuzalisha mafuta ya kupikia. Amesema hayo alipokutana kwa mazungumzo na wawakilishi kutoka Kampuni ya Mainland Group kutoka ya China Juni 24, 2024 jijini Dodoma. “Zao la alizeti ni miongoni mwa mazao…
