Tanzania kununua helikopta kuchunguza madini ardhini
Serikali ya Tanzania imesema ina mpango wa kununua helikopta itakayofungwa vifaa maalum vya uchunguzi wa madini ardhini. “Tutakwenda kununua helkopta ambayo tutaifunga vifaa vya utafiti kwa ajili ya ‘kuscan’ ardhi yetu kuweza kufahamu chini ya ardhi kuna nini,” ameeleza Waziri wa Madini Antony Mavunde. Waziri Mavunde anaeleza “bahati nzuri hivi sasa katika Dunia ya leo…
