Tanzania, Kenya kufanya mazungumzo kesho juu ya katazo la biashara pesatu.co.tz

Tanzania, Kenya kufanya mazungumzo kesho juu ya katazo la biashara

Nchi za Tanzania na Kenya zinatarajia kufanya mazungumzo juu ya katazo la biashara ndogo ndogo lililowekwa na Tanzania kwa wafanyabiashara wa kigeni. Katibu wa Baraza la Mawaziri, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Beatrice Askul aliiambia Kamati ya Bunge ya Ulinzi, Ujasusi na Mambo ya Nje Bunge kuwa kikosi cha wataalamu kipo Tanzania kujadiliana kuhusu kuondolewa kwa katazo hilo….

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2024 11 18 at 15.58.40 1

Nchi zilizoendelea zakumbushwa kutoa ahadi ya Dola bilioni 500

Nchi zilizoendelea zimetakiwa kutimiza ahadi yao ya kutoa dola za marekani bilioni 500, sawa na dola bilioni 100 kila mwaka kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2025. Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akichangia hoja…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 11 24 at 12.58.13

Afrika tujitegemee kifedha mabadiliko tabia ya nchi: Rais Samia

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka kwa Afrika kujitegemea katika fedha za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Rais Samia amesema hayo katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaojadili Masuala ya Tabianchi na Usalama wa Chakula Mkoani Arusha ulioandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki….

Soma Zaidi
sere

Serengeti yashinda tena

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeendelea kung’ara baada ya kushinda Tuzo ya Hifadhi bora Afrika kwa mwaka 2023 (Africa’s Leading National Park 2023) ikiwa ni mara ya tano mfululizo. Tuzo hiyo imetolewa na ‘World Travel Awards’ na kupokelewa na Mkuu wa Kanda ya Magharibi wa Tanapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Izumbe Msindai usiku wa…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2023 06 05 at 13.13.06

Vikwazo 10 vya kibiashara vyaondolewa Afrika Mashariki

Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuondoa vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs). Vikwazo nane vikiendelea kushughulikiwa, na vikwazo vingine vipya vinne vimewasilishwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara baina ya nchi hizo. Vilevile, nchi hizo zimekubaliana kutoza kiwango cha dola 10 za kimarekani kwa kilomita 100 kwa ajili…

Soma Zaidi
rrr

Chuo Kikuu kione aibu wahitimu wakichoma mahindi barabarani: Rais Ruto

Rais wa Kenya William Ruto amevitaka vyuo nchini humo kuzalisha wahitumu wanaoajirika. Amesema wanaangalia namna ya kuboresha kozi na aina ya ufundishaji katika vyuo na ubora wa wahitimu wanaozalishwa na vyuo husika. Rais Ruto amevitaka vyuo nchini humu kuboresha ufundishaji na kusema kama wanatumia pesa za umma, umma unatakiwa upate thamani kwa kila Shilingi ya…

Soma Zaidi
uuu

Marekani, Kenya zaongoza utalii Tanzania

Marekani na Kenya zimetajwa kuwa ndio nchi zinazoongoza kwa watalii wanaotembelea Tanzania. Utalii wa Tanzania umeanza kuongezeka ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia Januari mpaka Julai mwaka huu Tanzania imepata watalii 742,133 sawa na ongezeko la asilimia 62.7 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana ambapo kulikuwa na watalii 456,266. Kati ya watalii 742,133 walioingia nchini,…

Soma Zaidi
Enable Notifications OK No thanks