Msiwabanie vijana wajasiriamali: Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameagiza viongozi wa Mkoa wa Simiyu wasiwabane wajasiriamali, wawaelimishe na kuwapa miongozo ili wajiendeleze kiuchumi. Majaliwa alitoa agizo hilo Machi 26, 2023 wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Mji wa Bariadi katika eneo la stendi ya zamani akiwa njiani kwenda Maswa. Alitoa kauli hiyo akilenga biashara ya usafirishaji wa abiria…
