Fanyeni tafiti sekta ya wanyamapori: Chana

WhatsApp Image 2023 02 10 at 16.54.54

Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) imetakiwa kutumia weledi wake kufanya tafiti na kuja na matokeo ya tafiti hizo kwa wakati ili Wizara iweze kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili sekta ya wanyamapori nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema hayo Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi  ya TAWIRI,  Dkt. David Manyanza.
Amesema TAWIRI ni injini ya uhifadhi nchini hivyo inapaswa kuwajibika ipasavyo ili iweze kutoa  matokeo na majibu ya changamoto zinazoikabili sekta ya wanyamapori nchini.

Amesema matokeo ya tafiti za sensa ya wanyamapori  ambazo zimekuwa zikifanywa na TAWIRI zimekuwa zikitoa dira na  mwelekeo sekta ya wanyamapori nchini kujitazama iwapo inafanya vizuri  na mahali gani  juhudi ziongezwe ili wanyamapori waendelee kuwepo.

Amesema Tawiri lazima ifanye tafiti na kutoa majibu kwa wakati kwa kuwa ni Taasisi inayoonesha viashiria hatarishi kwa ustawi wa wanyamapori nchini Tanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. David Manyanza amemhakikishia Waziri kuwa katika kipindi chake cha uongozi moja ya kipaumbele chake ni kufanya tafiti kwa muda na kutoa matokeo ya tafiti hizo kwa muda ili Watanzania waendelee kunufaika na taasisi hiyo.

“Moja ya vitu tunavyojivunia ni kuwa na timu nzuri  ya wataalam wenye ushirikiano, nakuhakikishia tafiti tutakazozifanya zitazingatia weledi na kutolewa kwa muda muafaka”.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks