Umuhimu wa kuwa na akaunti ya benki
Kutunza fedha zako benki ni salama zaidi kuliko kutunza fedha taslimu nyumbani.
Mali zilizo kwenye benki ni ngumu kuibiwa ikilinganishwa na zile unazozitunza mwenyewe.
Hata hivyo ni muhimu kuzingatia kuwa unapohifadhi fedha zako katika benki fulani, una uwezo wa kupata pesa zako kila wakati, hata ikiwa wateja wote wataamua kutoa pesa zao kwa wakati mmoja.
Miamala mingi ya kifedha inahitaji uwe na akaunti ya benki ili:
Kutumia kadi ya benki.
Kutumia programu za malipo mbalimbali.
Kuandika hundi.
Kutumia ATM
Kununua mali mbalimbali kama viwanja, nyumba.
Kupokea mshahara kutoka kwa mwajiri wako.
Kupata riba kutokana na akiba yako.
Kuna Benki za Mtandaoni na Benki za Kawaida.
Unapofikiria kuhusu benki, labda unafikiria juu ya jengo. Hii inaitwa benki ya kawaida. Benki nyingi za kawaida pia zinaruhusu kufungua akaunti na kusimamia pesa zako mtandaoni.
Benki zingine ni za mtandaoni pekee na hazina majengo ambayo mteja anaweza kutembelea moja kwa moja na kupata huduma. Benki hizi kwa kawaida hutoa huduma sawa na benki za kawaida, isipokuwa wateja hawawezi kuzitembelea kupata huduma ana kwa ana.
Kuna aina mbalimbali za benki unazoweza kufungua akaunti kama vile:
Benki za rejareja: Hizi ndizo aina ya benki ambayo watu wengi wana akaunti. Benki za rejareja ni zile zenye lengo la kupata faida kwenye akaunti za akiba, mikopo au bima.
Benki za rejareja zinaweza kuwa na majengo ambayo unaweza kutembelea au zinaweza kuwa za mtandaoni pekee. Zaidi hutoa chaguzi zote mbili.
Vyama vya mikopo: Vyama vya mikopo hutoa akaunti za akiba, mikopo, na huduma zingine za kifedha, kama vile benki.
Vyama hivi vya mikopo huwa vinamilikiwa na wanachama wa vyama hivyo.
Vyama vya mikopo huwa na malipo ya chini na viwango vya riba vizuri kwenye akaunti za akiba na mikopo. Vyama vya mikopo wakati mwingine hujulikana kwa kutoa huduma bora zaidi kwa wateja.
Ni Aina Gani za Akaunti za Benki Ninaweza Kufungua?
Kuna aina tatu kuu za akaunti za benki ambazo mtu wa kawaida anaweza kufungua:
Akaunti ya akiba: Akaunti ya akiba ni akaunti ya amana yenye riba iliyoko kwenye benki au taasisi nyingine ya kifedha. Akaunti za akiba kwa kawaida hulipa kiwango cha chini cha riba, lakini usalama na uaminifu wake huzifanya kuwa chaguo zuri kwa kuweka pesa taslimu kwa mahitaji ya muda mfupi.
Zinaweza kuwa na vikwazo vya kisheria kuhusu mara ngapi unaweza kutoa pesa. Hata hivyo, kwa ujumla ni rahisi kutumia, hivyo ni bora kwa ajili ya kuweka akiba ya dharura au kuweka akiba kwa lengo la muda mfupi kwa mahitaji ya kifedha ama kununua mali mbalimbali kama viwanja na nyumba.
Akaunti ya kulipia: Akaunti ya kulipia pia ni akaunti ya amana kwenye benki au taasisi nyingine ya kifedha ambayo inakuruhusu kuweka na kutoa pesa. Akaunti za kulipia zina urahisi wa kutoa pesa, maana yake zinawaruhusu wateja kutoa pesa mara nyingi kwa mwezi (tofauti na akaunti za akiba au uwekezaji ambazo hazina urahisi huo), ingawa hazipati riba au zina riba kidogo sana.
Akaunti ya akiba yenye riba ya juu: Akaunti ya akiba yenye riba ya juu kwa kawaida hulipa kiwango cha riba cha juu zaidi kuliko akaunti ya kawaida ya akiba.
Faida ya kupata riba zaidi kwa pesa yako ni kwamba akaunti hizi za riba ya juu huwa zinahitaji amana kubwa za awali, kiwango cha chini cha salio, na malipo makubwa zaidi.
Kwa sasa dunia ipo kidigitali ambapo watu wanaacha kutumia pesa taslimu na kufanya manunuzi kidigital (cashless).
Watu wanatumia kadi za benki ama miamala kwenye mitandao ya simu kama Mix by Yas, M-Pesa, airtell money n.k. kufanya manunuzi ama malipo ya huduma mbalimbali.
Mbali na kuhifadhi fedha zao, zipo faida mbalimbali za kutotembea na fedha taslimu. Kufanya malipo bila fedha taslimu kunasaidia kurahisisha malipo, kuokoa gharama, usalama wa fedha zako na kuimarisha uchumi kidigitali.