Wananchi washauriwa kusajili vikundi vyao vya huduma ndogo za fedha

Screen Shot 2025 02 18 at 4.59.17 PM

Serikali imewashauri wananchi kusajili vikundi vyao vya huduma ndogo za fedha kupitia mfumo wa Wezesha Portal ambayo ni njia rahisi na haina gharama yoyote.

Ushauri huo umetolewa na, Afisa Usimamizi Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Jackson Mshumba wakati akitoa Elimu ya Huduma Ndogo za Fedha katika Kata ya Kibosho, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro.

Mshumba amesema kuwa Wezesha Portal ni jukwaa la dijitali lililoundwa kusaidia wajasiriamali na wafanyabiashara katika kukuza biashara zao, kupata mafunzo, na kupata rasilimali zingine za kuwasaidia kibiashara na inaokoa muda.

Screen Shot 2025 02 18 at 4.59.35 PMAidha, amesema kuwa kabla ya kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha ni vyema wananchi wanaotaka kuanzisha vikundi hivyo wakajiridhisha kuhusu wanachama wao wanaotaka kujiunga nao ili kuepukana na lawama na baadhi ya wajumbe kukimbia familia zao kutokana na madeni.

“Kabla ya kujiunga kwenye kikundi kitu cha kwanza lazima wawe wanatoka eneo moja ili kurahisisha utambuzi katika Serikali za Mitaa, pili, lazima waaminiane, tatu, wawe na lengo moja lililosababisha wao waamue kuanzisha kikundi,” amesema Mshumba.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks