Vijana 470 waitwa uhamiaji

anaa

Vijana 470 wamechaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji kwa nafasi ya konstebo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumamosi Februari 12, 2022 na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Mrajibu Paul Msele imesema vijana waliochaguliwa kujiunga wanatakiwa waripoti katika chuo cha uhamiaji kilichopo Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Februari 19, 2022.

Idara ya uhamiaji ilitangaza nafasi hizo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza, kidato cha sita na wa kidato cha nne kuomba nafasi hizo.

Kati ya nafasi hizo 470, 70 ni kwa walio na shahada ya kwanza, 100 kwa wale wa kidato cha sita na nafasi 300 kwa wale wenye elimu ya kidato cha nne.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2014, Idara ya Uhamiaji ilitangaza nafasi 70 na takribani vijana 10,000 waliitwa  kwenye usaili uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks