Tanzania kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu

WhatsApp Image 2024 05 03 at 14.01.58

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI anayeshughulikia Elimu Zainabu Katimba amsema serikali inatambua umuhimu na itaendelea kuboresha miundombinu ya Elimu ikiwemo Mabweni ya wanafunzi, uzio, majengo ya utawala na mabwalo kupitia miradi mbalimbali.

Katimba amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini Reuben Kwagilwa aliyetaka kujua, je ni lini Serikali itajenga bwalo la chakula, majengo ya utawala na mabweni ya wanafunzi katika Shule ya Sekondari Misima na Handeni?

“Kwa kutambua umhimu mkubwa sana wa miundombini hii katika shule zetu, Serikali itaendelea kutenga fedha kwenye bajeti kwaajili ya kuendelea kujenga miundombinu ya bwalo, majengo ya utawala, mabweni ya wanafunzi na uzio.

Hii ni katika Shule za Sekondari kote nchini zikiwemo Shule za Sekondari Misima na Handeni kupitia miradi mbalimbali ya elimu,” ameeleza Katimba.

Aidha, Katimba amesema Serikali inajenga shule 26 za bweni za wasichana za kitaifa katika Mikoa yote nchini kupitia mradi wa Sequip kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza zilijengwa katika Mikoa kumi na awamu ya pili zitajengwa katika Mikoa kumi na sita huku zikigharimu jumla ya shilingi Bilioni 4.1.

Katimba amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Innocent Edward Kalogeris aliyehoji ni lini Serikali itajenga shule maalumu ya Sekondari ya wasichana Dutumi katika Kata ya Bwakila, Morogoro vijijini.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks