Waziri Nape: kama unaamini umeibiwa kifurushi leta ushahidi
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kwamba uchunguzi uliofanya na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) umebaini kuwa hakuna wizi wa vifurushi vya mawasiliano ya simu unaofanywa. Waziri Nape amesema, kuna changamoto mbili kubwa kwenye matumizi ya simu janja ambapo, kwanza, mtumiaji anaweza kujiunga kifurushi cha intaneti, licha ya kuwa hatumii…
