Bandari kavu ya Kwala yaleta mapinduzi sekta ya uchukuzi
Uwepo wa Bandari Kavu ya Kwala katika eneo la Vigwaza, Mkoa wa Pwani, umeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya uchukuzi. Kutokana na mapinduzi hayo, msongamano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam umepungua na kurahisisha usafirishaji wa shehena kupitia reli na barabara kuu. Hayo yameelezwa Machi 16, 2025 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson…
