RC Dar apiga marufuku upangaji bidhaa za vyakula chini
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla amepiga marufuku utaratibu wa wafanyabiashara kuuza bidhaa kwa kuzipanga chini hususani bidhaa za chakula. RC Makalla ametoa onyo hilo wakati wa zoezi la usafi wa pamoja katika soko la Machinga complex mwishoni mwa wiki ambapo amewaelekeza viongozi wa masoko yote kudhibiti na kusimamia agizo Hilo….
