Rais Samia atangaza mkakati bei ya mafuta
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani ametangaza mkakati wa kubana matumizi ya Serikali katika bajeti ya matumizi ili kupata fedha za kupunguza makali ya ongezeko la bei ya mafuta nchini. Ongezeko hilo linalosababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali. Katika taarifa ya Rais Samia kwa vyombo vya habari Mei 9, 2022 amesema Serikali…
