WhatsApp Image 2024 11 19 at 16.33.01 1

Tanzania, Uturuki kushirikiana kukuza utalii

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Uturuki zimekubaliana kushirikiana kukuza Sekta ya Maliasili na Utalii lengo ikiwa ni kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchi hizo mbili. Hayo yameelezwa Novemba 19,2024 wakati wa kikao kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt. Mehmet Gulluoglu…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2024 11 18 at 15.58.40 1

Nchi zilizoendelea zakumbushwa kutoa ahadi ya Dola bilioni 500

Nchi zilizoendelea zimetakiwa kutimiza ahadi yao ya kutoa dola za marekani bilioni 500, sawa na dola bilioni 100 kila mwaka kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2025. Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akichangia hoja…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2024 10 24 at 13.30.34

Tathmini yaonesha uwepo wa madini katika eneo la hekari 7,180 mkoani Rukwa

Serikali kupitia Wizara ya Madini itaendelea kutangaza fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini zilizopo mkoani Rukwa, kutokana na uwepo wa Madini ya Ulanga, Shaba, Emerald, Titanium, Dhahabu, Hellium, Makaa ya Mawe na Aquamarine ili kuvutia wawekezaji na kuongeza tija katika uchumi wa mkoa huo. Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema hayo Oktoba…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2024 08 21 at 12.43.25

Serikali ya Tanzania inaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji, kodi: Mwigulu

Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi. Dkt. Nchemba ameyasema hayo Agosti 20, 2024 katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, wakati akiagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake…

Soma Zaidi
WhatsApp Image 2024 07 17 at 12.35.28

Rais Samia aahidi kufanya “Royal Tour” kuitangaza hifadhi ya Katavi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kufanya filamu nyingine ya Royal Tour katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi baada ya kujionea wanyamapori mbalimbali katika Hifadhi hiyo. Dkt. Samia ameyasema hayo Julai 15, 2024 wakati akizungumza na wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Mkoani Katavi. Kauli hiyo inafuatia ombi…

Soma Zaidi
Enable Notifications OK No thanks