Tutaendelea kujiimarisha kiuchumi: Majaliwa
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inajiimarisha katika kukuza uchumi wake kwa kutumia rasilimali zilizopo ili kuweza kumudu kutekeleza maeneo yote muhimu yakiwemo ya sekta ya afya, elimu na maji. Ameyasema hayo Februari 06, 2025 wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, George Mwanisongole katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma….
