Biashara kati ya Tanzania na China yafikia Dola Bilioni 8.78: Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na China umeendelea kukua ambapo mwaka 2023 biashara kati ya nchi hizo ilifikia dola bilioni 8.78. Amesema kuwa ukuaji na ushirikiano huo wa makampuni ya China na wafanyabiashara wa Tanzania umeleta maendeleo katika ukuaji wa viwanda vya ndani, kutengeneza ajira, ujenzi wa miundombinu…
