BoT: hatuna utaratibu wa mawakala uombaji leseni
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema haina utaratibu wa kuwataka waombaji wa leseni au usajili wowote kutumia washauri kwenye uandaaji na uwasilishaji wa maombi ya leseni. Taarifa ya BoT imesema imebaini uwepo wa taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojitangaza kuwa mawakala au washauri elekezi (consultant). “Tumebaini kuwa baadhi ya matangazo yanayotolewa na washauri sio sahihi…
