Serikali yatangaza fursa kilimo cha mbogamboga na matunda

WhatsApp Image 2024 02 29 at 17.02.43

Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde ametangaza fursa mbalimbali zilizopo Tanzania zinazohusu Sekta ya Kilimo, hususan kilimo cha mbogamboga na matunda pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali za kuwezesha uwekezaji na biashara nchini.

Silinde ametangaza fursa hizo katika maadhimisho ya Siku ya Tanzania Februari 28, 2024 wakati wa Maonesho ya Dunia ya Matunda na Mbogamboga (Expo 2023 Doha-Qatar) ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi 80 zinazoshiriki katika maonesho hayo.

Silinde ametembelea moja ya Supermarket kubwa kwenye jiji la Doha (Lulu Supermarket) na kujionea eneo la soko la mazao ya kilimo yakiwemo korosho, vitunguu, mbogamboga na matunda ambapo kuna mengi ya kujifunza kwa Tanzania, ikiwa ni pamoja na fursa ya soko kwa mazao yanayozalishwa nchini.

Naye Aseem Abdul Khader, Mkurugenzi wa Lulu Supermarket ameonesha utayari wa kupokea bidhaa mbalimbali za kilimo zinazozalishwa Tanzania ambapo Naibu Waziri Silinde amemuelekeza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Mohamed Omar kufanyia kazi furs hiyo kwa haraka.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks