Serikali kujishughulisha na kilimo cha muda mfupi kudhibiti dola

WhatsApp Image 2023 12 20 at 15.00.02

Katika jitihada za kudhibiti dola Serikali ya Tanzania imesema inajishughulisha na kilimo hasa cha muda mfupi ambacho kinazalisha mazao kwa haraka.

Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza hayo wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora (President’s Manufacturer of the year Awards – PMAYA) katika ukumbi wa Super Dome, Masaki.

Ameeleza kuwa mbali na kukua kwa sekta ya utalii nchini, Serikali pia imedhamiria kujishughulisha na kilimo cha muda mfupi ili kuthibiti dola nchini.

Katika hafla hiyo, Rais Samia amewataka wazalishaji wa bidhaa kupitia Shirikisho la wenye Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kuimarisha ubora wa bidhaa wanazozalisha.

Amesema serikali imeimarisha miundombinu ya barabara ba bandari ili bidhaa zinazozalishwa zisafirishwe nhje na kuingia nchini ili sekta ya viwanda iendelee kufanya vizuri.

Rais Samia amewataka wazalishaji kuongeza juhudi katika uzalishaji na uongezaji wa bidhaa (intermediate goods) ili kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

“Serikali inatarajia kuwasha kinu cha kwanza cha kufua umeme mwezi Januari 2024 katika bwawa kwa Nyerereikiwa ni jitihada za kuzalisha umeme wa kutosha ambao ni muhimu kwa wazalishaji,” ameeleza Rais Samia.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks