Rais Samia akaribisha wawekezaji wa India

WhatsApp Image 2023 10 11 at 16.01.32 1

Rais Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji wa India kuja kuwekeza Tanzania akiahidi mazingira rafiki ya biashara na maendeleo ya uchumi.

Mkuu huyo wa nchi, ameyasema hayo New Delhi wakati akizungumza na wawekezaji katika jukwaa la biashara na uwekezaji la Tanzania-India katika ziara yake ya siku tatu nchini India.

Rais Samia amesema Tanzania inatekeleza maendeleo na mageuzi ya uchumi ya Afrika yanayochochewa na sekta binafsi na uwekezaji katika kukuza uchumi.

“Kama sehemu ya mageuzi hayo, Tanzania tunatumia teknolojia ambayo inawawezesha wawekezaji kutoka nje ya nchi kuweza kusajili biashara zao kwa njia ya mtandao kabla ya kufika nchini,” ameeleza Rais Samia.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks