Rais Mwinyi afungua mkutano Benki ya Dunia

WhatsApp Image 2023 12 06 at 16.57.57

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania imeweka kipaumbele kuongeza uwekezaji katika elimu, afya, na huduma nyingine za kijamii pamoja na kilimo kinachozingatia hali ya hewa na mazingira.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Desemba 06, 2023 akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Tathmini ya muda wa kati wa mzunguko wa 20 wa Benki ya Dunia (IDA20 Mid Term Review) unaofanyika hoteli ya Golden Tulip, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.

Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kukuza uchumi na kupunguza umasikini.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema uchumi wa Zanzibar unanufaika na utalii wa kitamaduni ikiwemo Mji mkongwe ambao ni eneo la urithi wa dunia .

Vilevile Zanzibar ilipata msaada kutoka IDA fedha za kigeni dola za kimarekani Milioni 93 ili kuboresha upatikanaji wa huduma za mijini na kuhifadhi mazingira ya urithi wa kitamaduni.

Mkutano huo unaohusisha wakopaji, nchi wahisani na Menejimenti ya Benki ya Dunia unafanyika kuanzia Disemba 06 hadi 08, 2023.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks