Home KILIMO 1163 wathibitisha kushiriki Maonesho Nanenane 2025

1163 wathibitisha kushiriki Maonesho Nanenane 2025

0 comments 179 views

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli amesema kuwa washiriki wapatao 1163 wamethibitisha kushiriki katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane 2025 ambayo Kitaifa yanafanyika katika viwanja vya Nzuguni, mkoani Dodoma.

1163 wathibitisha kushiriki Maonesho Nanenane 2025. pesatu.com
“Kutakuwa na teknolojia za huduma za kisekta ambapo waoneshaji 753 wanatoka katika Sekta za Umma na Binafsi, washirika kutoka katika taasisi za nje ya nchi wapato 26, wajasiliamali 334, Vyama vya Ushirika 90 vikijumuisha wanachama wao pamoja na Vyama Vikuu vya Ushirika nchi nzima,” amefafanua Katibu Mkuu Mweli wakati akiongea na waandishi wa habari Julai 30, 2025, Nzuguni – Dodoma.

Maonesho ya Nanenane 2025 yanafanyika pia katika kanda saba nchi nzima ambapo yatahusisha washiriki mbalimbali wakiwemo wakulima, waongezaji thamani ambao ni viwanda, wafanyabiashara.

Wengine ni watafiti, washirika wa maendeleo, taasisi za fedha, kampuni mbalimbali za pembejeo na zana za kilimo na wale wanaohusika na usindikaji, ufungashaji na usafirishaji.

Katika tukio lingine, Katibu Mkuu Mweli amepokea hundi yenye thamani ya shilingi millioni 50 iliyotolewa kwa udhamini wa maonesho hayo kutoka Benki ya CRDB. Ameipongeza Benki hiyo kwa kuwa mdau muhimu wa kuchangia maendeleo katika Sekta ya Kilimo.

1163 wathibitisha kushiriki Maonesho Nanenane 2025. pesatu.com

Katibu Mkuu Gerald Mweli akipokea hundi yenye thamani ya shilingi millioni 50 iliyotolewa kwa udhamini wa maonesho hayo kutoka Benki ya CRDB.

Wageni rasmi katika Maonesho ni Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 8 Agosti 2025 katika kusherehekea Siku ya Nanenane.

Maonesho hayo, yanatarajiwa kufunguliwa na Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 01, 2025.

Kauli mbiu ni “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025.

Siku ya Mkulima ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1980 ambapo Serikali ya Tanzania ilianzisha maadhimisho hayo ili kutambua na kuthamini michango ya wakulima katika uchumi wa taifa.

Maonesho ya Nanenane ni hafla ya kila mwaka inayofanyika nchini Tanzania kuadhimisha siku ya wakulima, kuadhimisha mafanikio katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi. Hufanyika kuanzia Agosti 1 hadi 8 kila mwaka na huangazia maonesho na maonesho kutoka sekta mbalimbali zinazohusiana na Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ikiwa ni pamoja na ubunifu, teknolojia, na mazoea yanayolenga kuboresha tija na uendelevu.

Sherehe hiyo inatayarishwa na kuratibiwa na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa kushirikiana na Shirika la Chama cha Kilimo Tanzania (TASO) na kuhusisha Taasisi, Wizara na mtu mmoja mmoja wanaoshughulika na kilimo.

Miaka iliyopita sherehe hizi zilikuwa zikifanywa tarehe saba Julai kila mwaka na kuzingatia mafanikio makubwa na changamoto zinazokabili sekta ya kilimo inayowashirikisha wadau wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa.

Maadhimisho haya husherehekewa katika ngazi ya kanda ambapo kanda ya nyanda za juu za kusini zilifanyika viwanja vya John Mwakangale mjini Mbeya. Kwa kanda ya Kaskazini, sherehe zilifanyika viwanja vya Themi, Arusha, wakati kanda ya Mashariki zilifanyika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Morogoro na Kanda ya Ziwa, zilifanyika Mwanza, Viwanja vya Nyamhongolo na Kanda ya mwisho ni kusini, zilifanyika Ngongo katika Mkoa wa Lindi.

Katika mwaka wa 2024, Tanzania iliadhimisha maonyesho ya 31 ya Nanenane yakilenga kuongeza mwonekano wa kimataifa, kukuza ukuaji wa uchumi, na kukuza ushirikiano wa kimataifa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!