Dk. Mpango ataka maoni ya wafanyabiashara yazingatiwe

WhatsApp Image 2024 02 29 at 18.23.12

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango amewaagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, kuchukua maoni ya wafanyabiashara na wawekezaji ili kuboresha sera na sheria za kodi.

Ametoa agizo hilo Februari 27, 2024 wakati wa Jukwaa la Kodi na Uwekezaji jijini Dar es Salaam, ambapo amesema hatua hiyo itasaidia kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Dkt. Mpango amesema “kusanyeni na mtumie maoni ya wadau ili kuathiri upya mifumo ya kodi iendane na mabadiliko makubwa ya uchumi wa nchi.”

Akizungumza katika kongamano hilo, Prof. Kitila Mkumbo amesema Tanzania imekidhi vigezo vyote vya nchi inayovutia wawekezaji.

Amebainisha kuwa uzoefu wa uwepo wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa miaka 27, unaonesha nchi inayovutia uwekezaji lazima ikidhi vigezo kumi, ambavyo ni amani na utulivu, mazingira ya kisera na urekebu, utulivu wa kiuchumi na utulivu wa fedha kwa ujumla.

Vingine ni uwepo wa soko kwa bidhaa watakazozalisha wawekezaji, uwepo wa vipaji na nguvu kazi, ubora wa miundombinu, gharama ndogo za kuajiri wafanyakazi, viwango vya chini vya kodi, uwepo wa ardhi, na uwepo wa fedha za kugharamia miradi ya uwekezaji wa ndani.

Jukwaa hilo la Kodi na Uwekezaji linalofanyika kwa siku mbili ni fursa ya wafanyabiarasha na wawekezaji kutoa maoni na kushiriki mijadala inayolenga kuibua changamoto mbalimbali za kisera, kisheria ili kusaidia maboresho ya biashara na uwekezaji nchini.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks