Deni la Serikali ni Sh 82.12 trilioni

WhatsApp Image 2023 11 06 at 17.14.19

Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Juni 2023, deni la Serikali lilikuwa ni Sh 82.12 trilioni huku mikopo ikitumika kugharamia miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme, afya na elimu.

Waziri Nchemba amesema hayo Novemba 6, wakati akiwasilisha mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25.

Amebainisha kuwa tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Desemba 2022 inaonesha kuwa deni la Serikali limeendelea kuwa himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks