BoT yatoa ufafanuzi kuongezeka kwa riba
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema mwenendo wa Uchumi wa Dunia ulikuwa unaashiria uwepo wa Mfumuko wa bei kwa siku za mbele, hivyo ikaona ni vema iongeze Riba ya Benki Kuu (Central Bank Rate-CBR) kutoka asilimia 5.5 kwenda asilimia 6. BoT imeeleza hayo katika mkutano na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kutoa elimu…
