Home AJIRA Shirika la Reli Tanzania kumwaga ajira 2,460 mradi wa SGR

Shirika la Reli Tanzania kumwaga ajira 2,460 mradi wa SGR

0 comments 262 views

Shirika la Reli Tanzania linatarajia kuajiri wafanyakazi 2,460 katika mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kwa vipande viwili vya kutoka Dar es Salaam mpaka Makutopora.

Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya siku mbili ya bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR ) na MGR, kati ya Kigoma-Tabora na Tabora Mwanza iliyoanza Agosti 19, 2025.

Ajira hizo ni mbali na zaidi ya ajira 115,000 ambazo tayari zinatokana na mkandarasi katika kipande cha kwanza mpaka cha sita.

Shirika la Reli Tanzania kumwaga ajira 2,460 mradi wa SGR pesatu.comKatika ajira hizo 2,460 utekekezaji wake ni awamu ambapo katika mwaka wa fedha 2024/25 zaidi ya watumishi 500 wameshaajiriwa na mwaka huu wa fedha 2025/26 marajio ni kuajiri watumishi 272 na TRC itaendelea kuajiri kufikia watumishi 2,460.

Wakati utekekezaji wa utoaji ajira rasmi za Shirika ukiendelea, jumla ya ajira 115,000 kutoka mkandarasi zimesha wanufaisha Watanzania 115,000 zikiwemo za vijana wa elimu ya darasa la saba na viwango vingine vya elimu katika fani mbalimbali.

Mchanganuo wa ajira hizo 115,000 kutoka kwa mkandarasi ni kwamba ajira 35,000 ni za moja kwa moja na zaidi ya 80,000 ni zisizo za moja kwa moja zikijumuisha makundi mbalimbali kama baba na mama lishe, bodaboda, bajaji na watoa huduma za makampuni mbalimbali ya mawasiliano kama mocha, line za simu nk.

Soma: Tanzania, Congo kukuza biashara na uchumi

Utoaji wa ajira hizo ni utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya serikali kwamba miradi yote ambayo serikali imewekeza iwe na manufaa kwa Watanzania hususani wale wanaoishi kuzunguka miradi husika na wengine kutokana na ujuzi unaohitajika kwa viwango vya elimu na ujuzi wao.

Soma: SRG awamu ya kwanza kukamilika mwakani

TANZANIA NA SGR

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia shirika la reli Tanzania (TRC) imeazimia kujenga reli hii ya kisasa kueneza mtandao usiopungua km 2,561 ikiunganisha mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma, Katavi na nchi zinazokuwa na bandari (Rwanda, Burundi, DRC).

SGR ni reli ya kisasa na ya kwanza Africa mashariki na kati itakayokuwa na uwezo wa kupitisha treni zitakazoendeshwa kwa nishati ya umeme na yenye mwendo kasi usiopungua kilometa 160 kwa saa.

Lengo la reli hii ni kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji nchini ususani sekta ya reli ambapo yafuatayo yatarahisishwa;

  • Ongezeko la usafirishaji wa mizigo ambapo reli itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa maroli 500 ya mizigo.
  • Uokoaji wa muda kwa usafiri wa abiria na mizigo ambapo itasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
  • Ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali.
  • Oboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayo pitiwa na mradi.
  • Kuchochea maendeleo katika secta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususani katika maeneo ambapo reli hiyo inapita pamoja na kwa nchi jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na DRC.
  • Faida za kiuchumi kwenye sekta ya usafirishaji hasa kupunguza gharama za mara kwa mara za matengenezo ya barabara.

MUUNDO NA MPANGILIO WA RELI YA KISASA (SGR)

Reli hii ya kisasa inajengwa sambamba na reli iliyopo (MGR) isipokuwa maeneo maeneo machache yenye kona kali. Ujenzi wa reli hii unazingatia uhifadhi wa mazingira na usalama wa watu na mali zao.

  • Sehemu za mwingiliano wa magari na reli, kutakuwa na aidha kivuko cha juu na chini.
  • Uzio unajengwa kwa usalama wa watu na wanyama.
  • Elimu kuhusiana na usalama kwa ujumla itatolewa mara kwa mara.

Historia ya Shirika la Reli Tanzania inaweza kuanza kutajwa mnamo mwaka 1948 lilipoanzishwa Shirika la Reli na Bandari za Afrika Mashariki (EAR&H). Shirika la reli na bandari za Afrika ya Mashariki liliundwa mnamo mwaka 1948 sambamba na Jumuiya ya Afrika Mashariki na lilikuwa Shirika la umma lililosimamia reli na bandari za Kenya, Uganda na Tanganyika na baadaye Tanzania katika miaka kabla na baada ya uhuru wa nchi hizi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!