Tanzania kujifunza teknolojia magari ya umeme Singapore

WhatsApp Image 2024 10 23 at 11.28.54

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa Tanzania inayo nafasi kubwa ya kujifunza Teknolojia ya uwambaji wa magari (Assembling) yanayotumia umeme kutoka kiwanda cha magari cha HYUNDAI kwani ni rafiki kwa mazingira na hupunguza uchafuzi wa hali ya hewa.

Dkt. Biteko ameyasema hayo Oktoba 23, 2024 nchini Singapore mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni ziara mojawapo kwenye mkutano wa Wiki ya Nishati nchini Singapore na kusema kuwa Teknolojia kama hizo zina mchango mkubwa kwenye kuinua uchumi wa nchi na kuongeza pato la Taifa.

WhatsApp Image 2024 10 23 at 11.28.47“Nawapongeza sana wenzetu hasa kwa Teknolojia na ubunifu wa haya magari pamoja na Teknolojia ya Kilimo janja (smart farm) ambapo kwanza inatumia nafasi ndogo lakini matokeo yake ni makubwa sana,’’ amesema Dkt. Biteko.

WhatsApp Image 2024 10 23 at 11.28.51
Dkt. Biteko ashuhudia teknolojia ya kilimo janja (Smart farm) kinachotumia Teknolojia Mnemba

Kuhusu Teknolojia ya kilimo janja ambacho kinaendeshwa na kampuni ya ubunifu ya HYUNDAI kwa kutumia Teknolojia mnemba (Robot) Dkt. Biteko amesema, uwepo wa Teknolojia kama hii unaongeza tija, inapunguza gharama kwenye uendeshaji wake.

Naye, Makamu wa rais na Mkuu wa Biashara na mipango kutoka HYUNDAI Motor Group amesema mafanikio hayo yanayokana na kutumia fursa iliyopo wakati wa changamoto zilizokuwepo awali kama ya matumizi ya mafuta kwenye magari ambapo haikuwa rafiki kwa mazingira pamoja na uhaba wa maeneo kwa ajili ya kilimo nchini Singapore.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks