Rais Mwinyi: Tutaweka mkazo uzalishaji mwani Zanzibar

WhatsApp Image 2024 08 21 at 14.25.32

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali yake inakusudia kuweka mkazo zaidi kwenye sekta ya mwani ili kuzalisha bidhaa zenye ubora na kuzipatia soko la uhakika.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo Agosti 21, 2024, Ikulu Zanzibar wakati akizungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania Christine Grau.

Amesema asilimia 99 ya wakulima wa zao la mwani Zanzibar ni wanawake, hivyo amemueleza balozi huyo kuangalia haja ya kuwaunga mkono wanawake na wakulima wa mwani nchini, hasa kwa mafunzo na vifaa vya kisasa ili wazalishe mwani wenye ubora utakaoendana sambamba na soko la uhakika.

Mbali na mambo mengine ya maendeleo na uwekezaji ikiwemo utalii, Rais Dk. Mwinyi pia amemueleza Balozi Grau kuwa Uchumi wa Buluu ni sera kuu ya uchumi wa Zanzibar, hivyo amemueleza kuangalia fursa zinazotokana na sera hiyo.

Kwa upande wake, Balozi Christine Grau amesifu juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi na kueleza kuwa wanafanya kazi kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo kushirikiana na jamii kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa jamii Unguja na Pemba.

WhatsApp Image 2024 08 21 at 14.25.32 1
Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania Christine Grau.

Soma: Tanzania ya kwanza kilimo cha mwani Afrika


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks