Viwango vya malipo kwa waongozoza watilii, wapishi kuwekwa kisheria

WhatsApp Image 2023 11 07 at 12.39.29

Serikali iko kwenye mchakato wa kuweka malipo ya wapagazi, waongoza watalii na wapishi katika mlima kilimanjaro kuwa kisheria.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Dunstan Kitandula amesema hayo Bungeni Dodoma wakati akijibu swali lambunge wa Vunjo Dkt. Charles Stephen Kimei ambaye alitaka kujua lini Serikali itafanya mapitio ya viwango vya malipo ya ujira kwa wapagazi, wapishi na waongoza watalii katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Kitandula amefafanua kuwa Serikali inatambua changamoto ya viwango vya malipo ya ujira kwa wapagazi, wapishi na waongoza watalii katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Aidha, katika kutatua changamoto hizo, Wizara kwa kushirikiana na Vyama vya mawakala wa utalii yaani waajiri imeanza kutekeleza mikakati mbalimbali kwa ajili ya kufanya maboresho ya viwango hivyo vya malipo ya ujira.

‘‘ Wizara imefanya kikao na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na kujadili kuhusu viwango vya ujira kwa wapagazi, wapishi na waongoza watalii“ ameeleza Kitandula

Kitandula aliongeza kuwa Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inatarajia kufanya kikao kazi na wadau hao na waajiri wao kwa lengo la kupendekeza viwango stahiki ili viweze kuwasilishwa katika Bodi ya Utatu yenye dhamana ya kumshauri Waziri mwenye dhamana ili makubaliano hayo yawe ya kisheria.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks