Vivutio vya utalii Tanzania vyavutia Hispania

E51442C6 6686 4538 A1FA D837C5FF2EBC
Katika Maonesho ya Utalii ya FITUR yanayoendelea nchini Hispania, vivutio vya utalii vinavyopatikana nchini  vimewavutia washiriki wengi.
Kaimu Meneja wa Mikutano na Matukio wa Bodi ya Utalii (TTB) inayoratibu maonesho hayo kwa upande wa Tanzania Bi. Lily Fungamtama amesema kuwa wamepokea mawakala wengi wa utalii walioonyesha kuvutiwa na vivutio hivyo na kuweka miadi ya kuvitembelea katika siku za usoni.
Hispania ni miongoni mwa masoko makubwa yanayoleta watalii nchini ikiwa inashika nafasi ya 11 kwa kuleta watalii Tanzania.
Maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kwa siku tano.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks