TANZANIA YAFUNGUA MILANGO SWEDEN STOCKHOLM

Tanzania yafungua milango Sweden Stockholm . Katika jitihada za kuendeleza diplomasia ya uchumi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchanja mbuga barani Ulaya kwa kuonyesha fursa za uwekezaji Tanzania ambazo hazijaguswa. Hivi karibuni, Balozi wa Tanzania nchini Sweden,Mobhare Matinyi, ameongoza ujumbe wa kimkakati katika kikao kizito na wafanyabiashara pamoja na wawekezaji kutoka Chama cha Wafanyabiashara wa Sweden na Afrika (Swedish-African Chamber of Commerce).

Kikao hiki kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania jijini Stockholm, hakikuwa tu mkutano wa kawaida wa kidiplomasia. Kilikuwa ni jukwaa la kuuza rasilimali na mazingira bora ya biashara yaliyoboreshwa kwa kasi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kupitia mkutano huu, imebainika kuwa dunia sasa inaitazama Tanzania kama kitovu kikuu cha biashara Kusini mwa Jangwa la Sahara.

TANZANIA YAFUNGUA MILANGO SWEDEN STOCKHOLM -pesatu.co.tz

Serikali na Sekta Binafsi Kuunganisha Nguvu

Moja ya mambo yaliyovutia wawekezaji hao wa Sweden ni ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za serikali na sekta binafsi. Wakati Balozi Matinyi akiwa Stockholm, taasisi nyeti kutoka Dar es Salaam zilishiriki kwa njia ya mtandao kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu fursa za uwekezaji Tanzania.

Taasisi zilizoshiriki ni pamoja na:

  • TISEZA: Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi.
  • BoT: Benki Kuu ya Tanzania (kuhusu sera za kifedha).
  • TRA: Mamlaka ya Mapato Tanzania (kuhusu motisha za kodi).
  • BRELA: Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni.
  • TPSF & TNCC: Wawakilishi wa sekta binafsi nchini.

Ushiriki wa taasisi hizi ulihakikishia wawekezaji wa Sweden kuwa mchakato wa kuanza biashara Tanzania sasa ni rahisi, wa kidijitali, na usio na urasimu usio wa lazima.

TANZANIA YAFUNGUA MILANGO SWEDEN STOCKHOLM -pesatu.co.tz

Dira ya Maendeleo 2050 na Mwelekeo wa Rais Samia

Balozi Matinyi alikazia kuwa fursa za uwekezaji Tanzania zimejikita kwenye misingi ya Dira ya Maendeleo ya 2050. Balozi alirejea hotuba tatu muhimu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo zinatoa dira ya nchi:

  1. Hotuba ya uzinduzi wa Bunge la 13 (Novemba 14, 2025).
  2. Hotuba kwa Mabalozi katika Ikulu ya Chamwino (Januari 15, 2026).
  3. Hotuba ya Dubai kwenye Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji Afrika (GAIS) (Februari 5, 2026).

Ujumbe wa Rais Samia uko wazi: Tanzania ni nchi yenye utulivu wa kisiasa, sheria zinazotabirika, na inayojali maslahi ya mwekezaji na mzawa kwa pamoja.

Sekta Muhimu Zinazovutia Macho ya Dunia

Tanzania haitafuti tu mwekezaji, bali inatafuta washirika wa maendeleo katika sekta ambazo zina tija kubwa. Katika wasilisho lake, Balozi Matinyi ametaja maeneo makuu kumi (10) ambayo ni uti wa mgongo wa fursa za uwekezaji Tanzania kwa sasa:

  1. Nishati: Uzalishaji wa umeme wa uhakika.
  2. Viwanda: Kuongeza thamani ya malighafi zetu.
  3. Kilimo-biashara: Tanzania kama ghala la chakula la Afrika.
  4. Uchumi wa Buluu: Matumizi endelevu ya rasilimali za bahari.
  5. Uchumi wa Kidijitali: Mapinduzi ya teknolojia na mawasiliano.
  6. Madini ya Kimkakati: Graphite, Nickel, na madini mengine ya teknolojia mpya.
  7. Misitu na Utalii: Kuendelea kuwa kivutio namba moja duniani.
  8. Miundombinu na Usafirishaji: SGR na bandari zetu zinazounganisha nchi nane zisizo na bandari.
TANZANIA YAFUNGUA MILANGO SWEDEN STOCKHOLM -pesatu.co.tz

Mafanikio ya Papo Hapo: Kampuni za Sweden Kuanza Kazi

Haikuchukua muda mrefu baada ya kikao hicho, kampuni kadhaa kubwa za Sweden zimeanza majadiliano ya awali na ubalozi. Sweden, ikiwa ni nchi inayoongoza barani Ulaya katika teknolojia ya kijani, imeonyesha nia ya dhati kuleta teknolojia ya uzalishaji wa umeme kwa kutumia taka (Waste-to-Energy). Hii ni fursa adhimu kwa miji inayokua kama Dar es Salaam na Dodoma kutatua changamoto ya taka huku ikizalisha nishati.

Pia, kuna nia kubwa katika utengenezaji wa vifaa vya tiba. Hii itaifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za afya kanda ya Mashariki na Kati, ikipunguza gharama za kuagiza vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

TANZANIA YAFUNGUA MILANGO SWEDEN STOCKHOLM -pesatu.co.tz

Ziara ya Kihistoria: Septemba na Oktoba 2026

Ili kuhakikisha maneno yanageuka kuwa vitendo, kikao kiliazimia kuandaa safari maalum ya wafanyabiashara wa Sweden kuja nchini Tanzania mwezi Septemba au Oktoba mwaka huu. Safari hii itaratibiwa na Ubalozi, jumuiya ya wawekezaji ya Sweden, na Shirika la Ndege la Qatar (Qatar Airways). Lengo ni kuwaleta wawekezaji hawa “field” ili wajionee wenyewe utulivu na uchumi unavyopaa.


Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading

Enable Notifications OK No thanks