Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) limepongezwa kwa juhudi kubwa inazofanya za kutangaza vivutio vya utalii.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea banda la TANAPA wakati akifungua rasmi maonesho ya 9 ya biashara yanayofanyika jijini Tanga.
Maonesho haya yanaendelea hadi tarehe 6/6/2022.
Sekta mbalimbali, mashirika ya serikali na binafsi yanashiriki kwenye maonesho haya.
Pia, Mkuu wa mkoa wa Tanga Adam Malima amehudhuria ufunguzi wa maonesho ya 9 ya biashara katika jjiji la Tanga.
Discover more from PesaTu – Habari za Biashara na Uchumi Tanzania
Subscribe to get the latest posts sent to your email.

