Tanzania ya kwanza kilimo cha mwani Afrika
Asilimia 90 ya mwani unaolimwa katika visiwa vya Zanzibar unalimwa na wanawake. Kilimo hichi cha baharini, kimewainua wanawake wengi visiwani humo kiuchumi kutokana na biashara hiyo kukua kwa kasi. Afisa Mawasiliano Idara ya Maendeleo ya Uvuvi na Mazao ya Bahari kutoka Wizara ya Uchumi wa Buluu Zanzibar Semeni Salum anasema kilimo hicho kimechochewa na jitihada…
