Tanzania inatumia Bilioni 19.5 kuagiza mchuzi wa zabibu
Tanzania hutumia takribani shilingi Bilioni 19.5 kila mwaka kuagiza wastani wa lita milioni 10 za mchuzi wa zabibu nje ya nchi ili kukidhi mahitaji ya ndani. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema hayo Agosti 19, 2024 wakati akizindua kiwanda cha kusindika zabibu kilichopo Chinangali II, Wilaya ya Chamwino…
