Gavana Tutuba akutana na Balozi wa Uingereza
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Marianne Young, katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam, tarehe 29 Aprili 2025. Katika mazungumzo hayo, Gavana Tutuba alieleza kuwa uchumi wa Tanzania umeendelea kuimarika licha ya changamoto mbalimbali za kiuchumi duniani. Alibainisha kuwa…
