Tunaendelea kuboresha mazingira ya biashara: Serikali
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru, amewahakikishia wafanyabiashara na makampuni binafsi kwamba Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuwawezesha kuendelea kuwekeza na kukuza uchumi wa nchi. Mafuru ametoa ahadi hiyo wakati wa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Takashi Araki. Amesema Sekta Binafsi ina imani…
