Hakuna kiwanda kitakachofungwa: Waziri Kijaji
Waziri wa Uwekezaji , Viwanda na Biashara , Dk Ashatu Kijaji amesema serikali imedhamiria kuona viwanda vyote nchini vinafanya kazi kwa siku zote saba za wiki. Ameongeza kuwa hakuna kiwanda kitakachofungwa kwa kushindwa kujiendesha kutokana na masharti ya uwekezaji au kukosa masoko ya bidhaa wanazozalisha. Dk Kijaji amesema hayo alipotembelea kiwanda cha 21 st Century Textile LTD kilichopo…
