Kibegi, jezi za Simba zilizopandishwa Ml. Kilimanjaro zaleta Sh 29m
Klabu ya Simba imefanya mnada wa kibegi na jezi zilizopandishwa Mlima Kilimanjaro kwa Sh29 milioni. Jezi hizo za msimu wa mashindano 2023/24, zilizinduliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro Julai 21, 2023. Jezi hizo za aina tatu ambazo zimepigwa mnada ni zenye majina ya viongozi, Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi….
