Tanzania, Italy watia saini mkataba wa 1bn
Tanzania na Italia, kupitia Shirika lake la Maendeleo (AICS), zimetia saini mkataba wa msaada wa Euro 410,000 (sawa na shilingi Bilioni 1). Msaada huo ni kwa ajili ya programu ya kuimarisha mfumo wa takwimu na usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano mkoani Tanga. Mkataba huo umetiwa saini katika Ofisi za Hazina…
