Watanzania watakiwa kuwa na uthubutu
Watanzania wametakiwa kuwa na uthubutu wa kufanya biashara na kuwekeza katika maeneo mbalimbali badala ya kutegemea watu kutoka nje ya nchi katika uwekezaji. Ally Dahal, ambae ni Mkurugenzi wa Jochata Vocational Centre ametoa wito huo katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba jijini Dar es Salaam. “Watanzania wengi hawana uthubutu wa kuanzisha biashara,…
